Video na makala nyingine inayoonyesha jinsi ya kufanya kilimo cha nyanya

Leo nimekuwekea post nyingine inayoelezea zaidi kuhusu kilimo bora cha nyanya ili uweze kujipatia kipato zaidi na kuboresha maisha yako. Pia nimekuwekea na video inayoelezea namna ya kufanya kilimo hicho



KILIMO BORA CHA NYANYA

Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani. Kwa Tanzania, nyanya ni zao la kwanza katika mazao ya mboga linalo limwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha na mboga zingine. Nyanya hutumika karibu Katika kila mlo. Kulingana na umuhimu wa zao hili kama chakula na pia kama zao linalomwingizia kipato Mkulima, kuna haja ya kutoa mafunzo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wake. Pia kuna umuhimu wa kufundisha wakulima kutoka sehemu zingine wasiolima zao hili ili nao waweze kuzalisha nyanya na hivyo kuongeza idadi ya aina za mboga katika maeneo yao.
MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA
Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa maua na matunda. Zao hili hupenda kipindi kirefu cha jua na joto ili kuongeza ukuaji wa matunda na kupunguza magonjwa ya aina ya ukungu/kuvu. Zao hili halipendi mvua nyingi ingawa linahitaji maji kwa wingi. Katika kipindi chenye mvua nyingi na jua kidogo nyanya hushindwa kutoa maua na matunda ya kutosha bali huweka majani mengi. Katika kipindi hiki pia, nyanya hushambuliwa sana na magonjwa ya ukungu. Nyanya hupendelea udongo unaopitisha maji kwa urahisi na wenye rutuba ya kutosha na hivyo hupenda samadi. Udongo uwe umetifuliwa vya kutosha kuruhusu mizizi kushika vema.
AINA ZA NYANYA
Kuna aina kuu mbili za nyanya kulingana na ukuaji wa mmea: yaani nyanya inayo refuka zenye kuhitaji egemezi (mfano Money maker) na aina ya pili ni nyanya fupi zenye kutoa matawi mengi mfano Roma na Cal J.

UKUAJI WA MICHE
Miche ya nyanya huzalishwa kwenye kitalu kwa kupanda mbegu. Mbegu za nyanya huota baada ya siku 5 hadi 10. Baada ya kukua kitaluni kwa muda wa wiki 4 hadi 5 toka kuota kwa mbegu, miche hupandwa shambani. Kabla ya kupandikiza shambani miche huandaliwa kwa kupunguza umwagiliaji maji kwa siku moja au mbili ili miche izoee hali ngumu kabla ya kuhamishiwa shambani. Hapo shambani miche hupandikizwa kwa kuzamishwa katika kina kirefu zaidi ya ilivyo kuwa kitaluni. Hii inasaidia miche kutoa mizizi ya pembeni mingi zaidi kwa ajili ya kufyonza maji pamoja na virutubisho aridhini. Baada ya kupandikiza mwagilia maji ya kutosha. Usimwagilie maji juu ya mche wa nyanya. Katika kipindi cha jua kali, tandaza nyasi kwenye tuta ili kupunguza upotevu wa maji na unaweza kuweka kivuli kwa kutumia majani ya miti au migomba. Kulingana na aina ya nyanya na rutuba ya udongo, nafasi ya kupandia ni sm 60 kati ya mstari hadi mstari na 45 hadi 60 nafasi ya mche hadi mche. Kama udongo hauna rutuba ya kutosha inapendekezwa kutumia nafasi kubwa ya kupanda.
UTUNZAJI
Nyanya fupi zisizo refuka kwenda juu, ni rahisi sana kutunza na hazihitaji huduma nyingi. Tatizo kubwa ni kuwa kwa kutambaa chini, katika kipindi cha mvua huwa karibu na magonjwa yatokanayo na udongo. Katika kipindi cha jua kali, matunda huungua kwani mmea huwa na majani machache tu yanayo kinga matunda yasipigwe na mionzi ya jua.
MBOLEA
Licha ya mbolea ya kupandia, unashauriwa kuongeza mbolea kipindi cha wiki mbili au tatu baada ya kupandikiza miche bustanini. Mbolea hii ya kukuzia iwekwe kuzunguka shina la mmea kwa umbali wa sentimeta 5 hadi saba kutoka kwenye shina. Kwa mbolea kama vile CAN, NPK, au SA tumia kifuniko kimoja cha soda kwa shina. Mbolea hii inaweza kuwekwa mara mbili kabla ya mvuno wa kwanza. Ili kurefusha kupindi cha uzaaji wa zao la nyanya (na hata mazao mengine yatoayo matunda kama vile nyanya chungu, biringanya, pilipili hoho, nk) inapaswa kuongezea mbolea katika kipindi cha uvunaji mfano baada ya kuvuna mara mbili unashauriwa kuongeza mbolea ya samadi na mbolea kama vile NPK. Hii inasaidia mmea kuendelea kutoa maua bila kuchoka. Kwa kawaida nyanya fupi jamii ya “Roma” huweza kuzaa na kuvunwa kwa kipindi cha wiki 6 hadi 8 tu. Lakini kama utakuwa unaongezea mbolea na kukazania matunzo ya bustani (hasa usafi wa bustani na Kumwagilia maji ya kutosha), nyanya zinaweza kuendelea kuzaa kwa muda mrefu zaidi. Hii ni tofauti
na mazoea ya wakulima wengi kuwa mara nyanya zianzapo kuzaa huduma za palizi na usafi wa shamba huachwa na kutilia maanani kazi ya kuvuna pekee. Hii inajitokeza zaidi kwenye aina ya nyanya fupi.
Kwa nyanya fupi ni vizuri kuhakikisha kuna matawi mengi iwezekanavyo ili kuweza kupata matunda mengi zaidi. Hivyo usipunguze matawi katika aina hii ya nyanya. Kwa nyanya ndefu zenye kuhitaji egemezi,tunashauriwa kukuza nyanya kwa tawi moja lisilo na vichipukizi pembeni au matawi mawili na kuacha mnyanya urefuke.
Kupunguza majani ni muhimu pia katika kupunguza maambukizo ya ukungu katika shina na pia kutoa nafasi ili
mwanga kupenya na kuruhusu mzunguko wa hewa. Majani yapunguzwe kipindi cha asubuhi kwa kutumia mkono na siyo kisu kwani kinaweza kueneza magonjwa kutoka mche hadi mche. Kwa nyanya ndefu, majani ya chini ya matunda huondolewa kadiri unavyo endelea kuvuna. Unashauriwa upunguze majani wakati wa asubuhi kwa kutumia mkono na pia usitoe zaidi ya majani matatu katika mmea kwa mara moja.
UMWAGILIAJI
Nyanya ni zao linalohitaji maji mengi sana kwa ajili ya ukuaji wa mmea na matunda yake. Umwagiliaji uwe wa kulingana kwa kila siku iliyo pangwa. Usibadilishe ovyo kiasi cha maji na ratiba ya kumwagilia. Hii inasababisha kuoza kwa kitako cha nyanya. Pia ili kutunza maji katika udongo, inashauriwa kuweka matandazo katika mzunguko wa shina la nyanya au bustani yote. Nyanya inayo kua vizuri hutumia maji lita mbili kwa siku
katika kipindi cha jua kali. Hivyo katika umwagiliaji ni busara kuzingatia kiasi hiki cha maji katika kipindi kama hiki. Pia kama unatumia keni, mpira au bomba usimwagilie maji juu ya matawi ya nyanya kwani umwagiliaji wa namna hii utasababisha kuenea kwa magonjwa ya ukungu.
MATATIZO YA KILIMO CHA NYANYA
Matatizo yanayosumbua kilimo cha zao hili ni magonjwa na wadudu waharibifu. Hapa tutajifunza mbinu mbali mbali za kuzuia magonjwa na wadudu waharibifu.
WADUDU WAHARIBIFU
FUNZA WA NYANYA (Funza wa vitumba)
Huyu funza hushambulia mazao mengine kama vile pamba, mahindi, mtama, maharage n.k. Mdudu huyu hushambulia matunda ya nyanya kwa kutoboa na hivyo kuyafanya yapoteze soko kwasababu hayafai kuuzwa katika soko na pia yanaweza kuoza wakati wa usafirishaji. Ili kuthibiti piga dawa ya kuua wadudu kama vile thiodan, sevin ya unga, karate, selecron, n.k. Muarobaini hutumika pia katika kupunguza uharibifu wa mdudu huyu.
INZI WEUPE
Wadudu hawa huruka ruka kwenye shamba la nyanya na kukaa chini ya majani. Mdudu huyu hueneza magonjwa ya virusi kama vile “ukoma wa nyanya”. Usafi wa shamba na mazingira ya yake ni muhimu katika kupunguza kuzaana kwa wadudu hawa. • Ili kuthibiti wadudu hawa kwenye bustani ya mboga na pia katika maficho yao, piga dawa kama vile karate, cypermethrin mara kwa mara. • Panda mimea mingine (kama vile tumbaku) inayo vutia wadudu hawa kwenye maeneo ya bustani kisha piga dawa katika miche ya tumbaku ili kuwaangamiza kwa wingi.
MINYOO
Mdudu huyu hukaa kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha. Huvamia mizizi ya nyanya na kuharibu mfumo wa usafirishaji maji na chakula kwenye nyanya iliyo athirika. Uking'oa mche wa nyanya utaona vifundo kwenye mizizi.
KUZUIA
Mbinu za kuthibiti ongezeko la wadudu hawa ni kuharibu hali ya udongo inayo mfanya aishi na kuzaana. Mbinu hizi ni: • Kulima shamba kwa kutifua baada ya kuvuna nyanya ili udongo wa chini ukae juani na kukauka. Hii inasaidia kuangamiza wadudu hawa kwa joto na ukosefu wa maji. • Choma moto na kuteketeza mabaki ya nyanya baada ya kuvuna. • kuzungusha aina ya zao la nyanya au jamii ya nyanya na mazao mengine yasiyo vamiwa na adui huyu. Hii huwafanya minyoo wasipate hifadhi na chakula kutoka kwenye mimea wanayo tumia kuishi na kuzaliana. Hivyo idadi yao kupungua katika udongo. • kabla ya kupanda zao weka samadi nyingi katika udongo kwenye eneo lililo athiriwa na wadudu hawa kwani hawapendi udongo wenye samadi nyingi. • Panda manung'a nung'a (Tagetes spp) katika eneo lililoathirika na minyoo hawa, mimea hii hutoa sumu ya aina fulani ambayo huathiri ukuaji na kuzaliana kwa minyoo hawa.
MAGONJWA
Uchunguzi umeonyesha kuwa katika maeneo ya Kilombero na Gairo, nyanya na mazao mengine jamii ya nyanya ndiyo hushambuliwa sana na magonjwa kuliko mazao mengine ya mboga.
UKUNGU
Huu ni ugonjwa unaopenda hali ya unyevu mwingi hewani. Hivyo hujitokeza zaidi wakati wa masika. Pia sehemu zenye umande mwingi wakati wa usiku, ugonjwa huu hujitokeza hata wakati wa kiangazi.
DALILI ZAKE
Ugonjwa huu hushambulia shina, maua na matunda. Kuungua kwa majani kama vile yamechomwa na maji moto. Chini ya jani utaona unga unga mweupe. Matunda pia hushambuliwa na ugonjwa huu na hugeuka kuwa meusi na magumu.
KUZUIA
• Inabidi kuchanganya mbinu mbali mbali za kupambana na ugonjwa huu. • Kwanza ni usafi wa shamba kwa jumla yaani hakikisha unaondoa magugu katika bustani. • Tandaza nyasi juu ya matuta yaliyo pandwa nyanya. • Ondoa majani yaliyo zeeka na yanayo onyesha dalili za ugonjwa huu. katika kupunguza majani, hakikisha sehemu za chini ya mmea ni wazi na kuna mzunguko mzuri wa hewa. Punguza majani katika mmea ili kupunguza umande na ukungu kwenye mmea. • Baada ya kupunguza majani na machipukizi hakikisha unatupa mbali majani hayo na siyo kuyaacha kwenye tuta la bustani. • Ondoa kabisa mmea ulio na dalili za ugonjwa huu • Kupiga dawa katika kipindi cha mvua mara baada ya mvua kubwa. Fanya hivyo mara moja au mara mbili kwa wiki kutegemea na wingi au mfululizo wa mvua. Unapoona jua limetoka piga dawa ili ugonjwa usijitokeze tena. Baadhi ya madawa yanayofaa kukinga ugonjwa huu ni Dithane M45, Bravo, Benlate , Ridomil, Topsin n.k. Kumbuka kuwa kila
mwaka madawa yenye nguvu zaidi hutengenezwa, hivyo uliza watalaam walioko karibu nawe. Ingawa Blue Copper inauzwa kwa bei nafuu, nguvu yake in kidogo sana kuthibiti huu ugonjwa. Muarobaini pia unaweza kutumika kupunguza ugonjwa huu. Changanya unga unaotokana na mbegu za muarobaini kiasi cha nusu kilo ya unga katika lita 20 za maji.
UKOMA WA NYANYA
Huu ni ugonjwa wa virus unao enezwa na inzi mweupe. Inzi hawa hushambulia zaidi nyanya wakati wa kiangazi, hasa kipindi cha joto kali.
DALILI
• Majani machanga hujikunja na baadaye majani yote. • Kupungua kwa utoaji maua na matunda na hata yakitokea matunda huwa ni madogo. • Mmea kudumaa na kutozaa kabisa.
KUZUIA
Mbinu madhubuti ni kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu kwenye shamba kwa kudhibiti kuzaana na kuenea kwa mdudu (inzi mweupe) kama tulivyo ona katika kupambana na mdudu huyo, yaani: • Kuondoa mimea michache iliyo shikwa na ugonjwa maana wadudu hawa wanachukua ugonjwa huu kutoka mimea hii. • Kutumia mbegu zilizo hakikishwa kuwa zinaweza kuvumilia ugonjwa huu na kutoa mavuno mazuri. • Usilime nyanya karibu na eneo lililo na mazao kama bamia,mipapai maana mimea hii huhifadhi inzi mweupe. Kuua inzi weupe wanaofyonza nyanya na kusambaza virusi kwa kutumia madawa. Tumia madawa kama vile Selecron, Decis, Karate n.k. • Epuka kuchanganya zao la nyanya na mazao mengine yanayohifadhi hawa nzi kama vile mipapai na bamia. • Ng'oa na kuchoma moto mimea yote iliyougua ugonjwa huu.
UGONJWA WA KUOZA SEHEMU YA SHINA INAYOGUSA UDONGO NA MMEMA KUNYAUKA KAMA UMEKOSA MAJI
• Wadudu wanaosabisha ugonjwa huu hupatikana ardhini. • Hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huu baada ya dalili
kujitokeza. • Kupiga madawa za viwandani ardhini kabla ya kupanda nyanya husaidia kupungu wadudu wa ugonjwa. • Epuka kupanda nyanya au mazao jamii ya nyanya katika eneo moja kwa muda mrefu mfulilizo. Baadhi ya mazao yanayohusiana na nyanya ni bilinganya, pilipili, ngogwe, mnavu, n.k.

Ugonjwa wa miche michanga ya nyanya kuoza sehemu ya shina inayogusa udongo na kufa ghafla
Ugonjwa huu hushambulia miche kitaluni na husabishwa na wadudu waishio ardhini. Mara baada ya dalili, ugonjwa huu hauna dawa ila unaweza kukingwa kwa kutumia njia zifuatazo: • Choma moto udongo wa kutengenezea kitalu kabla ya kupanda mbegu zako. Kutumia mboji husaidia kukinga miche dhidi ya ugonjwa huu. • Epuka kumwagilia maji kupita kiasi na kutumia kuvuli kizito
MATUNDA YA NYANYA KUOZA KITAKO
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na: • Umwagiliaji wa nyanya bustanini usio na mpangilio maalumu. Mfano, kumwagilia mimea maji mengi kisha kuiacha bila maji kwa siku kadhaa. • Upungufu wa virutubisho aina ya chokaa. Dalili zake ni matunda ya nyanya kuoza sehemu ya kitako na kuonyesha rangi nyeusi. Kuzuia ugonjwa huu, zingatia kuwa na utaratibu mzuri wa kumwagilia maji ambao haubadiliki ovyo kiratiba na kiasi cha maji
yanayowekwa. Rutubisha mimea kwa madini ya chokaa kwa kutumia mbolea aina ya CAN zenye madini haya.
UPUNGUFU WA WADINI YA FOSFPRASI

VIDEO YENYEWE HII HAPA ITAZAME

Jinsi ya kufanya kilimo cha nyanya ili uweze kujipatia kipato cha kutosha

Utangulizi:

Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.

Uzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania

Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na Marekani, Italia na Mexico. Kwa upande wa Afrika nchi zinazo lima ni kama; Malawi, Zambia na Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Afrika Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania.

Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania. Uzalishaji wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni jumla ya tani 129,578 ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya mboga. Kwa mujibu wa Wizara ya kilimo ya Tanzania maeneo yanalolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida. Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari 15,398). Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana. 

Full Video: Angalia Jinsi ya kufanya kilimo cha papai

Papai ni tunda lenye ladha nzuri, na rahisi kuliwa. Aina hii ya tunda ni chanzo cha virutubisho muhimu mwilini, ambavyo husaidia kujenga mwili.Zao hili asili yake ni ukanda wa kitropiki ambao hauna baridi kali na joto kiasi.

Papai ni moja ya matunda ambayo huchukua muda mfupi hadi kufikia mavuno. Huchukua muda wa miezi 8-9 kufikia mavuno. 
Matunda katika mpapai utokeza katika kila jani na mpapai kwa wiki moja unauwezo wa kutengeneza majani mawili na kwa makadilio mpapai huanza kutengeneza maua katika jani la 32 hii ikimaanisha ni baada ya wiki nne.

FAIDA KIUCHUMI
Hekari moja inauwezo wa kuwa na mipapai 1000-2500. Mavuno ya mapapai kwa miezi 8 - 9 kwa mavuno ya kwanza ni tani 40 - 60 ikiwa kila mpapai unaweka matunda 40 hadi 50 kwa miezi 8 - 9. Baada ya mavuno ya kwanza, mavuno ya mapapai hayana msimu hivyo yataendelea ndani ya miaka mitano katika uangalizi mzuri wa mipapai yako hadi kufikia kipindi ambacho mpapai wako utapokufa..

DOWNLOAD KITABU: Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Matumizi ya Matunda na Mboga baada ya kuvuna

Kuna kitabu kinachoweza kukusaidia kupata mafunzo ya kuongeza thamani ya mazao uliyozalisha ili kujiongezea zaidi kipato. Sio lazima ukishavuna mazao yako ukapeleka moja kwa moja sokoni.

Inawezekana kujiunga katika vikundi vya watu ambao mnazalisha mazao yanayofanana kwa ubora unaolingana na hatimaye kuyaongezea thamani.

ZIJUE FAIDA ZA KUTUMIA MATANGO KWA AFYA YAKO

Watu wengi tunapenda matunda Fulani kwa ladha yake tuu bila kutaka kupata faida, katika mwili ikiwa faida ya baadhi ya matunda ni pamoja na  radha yamatunda  mabalimbali.

1.    Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B.
2.    Tango huupa mwili na vitamin. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.

3.    Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa machoni na kuondoa vimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani tango lina virutubisho vya kuondoa vimbe hizi na pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.

FAIDA ZITOKANAZO NA MATUMIZI YA MAPAPAI

ASILI ya mpapai ni Amerika ya Kati, ambapo kuanzia matunda, majani na utomvu wa mmea huu hutumiwa kama dawa maeneo mbalimbali duniani. Vile vile, matunda na utomvu wake yamekuwa yakitumika kutengeneza pombe na mvinyo katika baadhi ya nchi, huku wengine wakitumia mpapai kama dawa kwa mifugo na binadamu.
Inaelezwa kuwapo na tafiti zilizowahi kufanyika na kuchapishwa katika jarida lijulikanalo kwa jina la ‘Archieve’ la nchini India mnamo Oktoba 27 mwaka 2010, ambapo jarida hilo lilieleza kwamba juisi ya majani ya mpapai iliweza kusaidia wagonjwa watano waliowahi kupata homa ya dengue.


Mbali na utafiti huo, pia kuna tafiti zilizowahi kufanywa na madaktari wa nchini Marekani na Japani na kubaini kuwa, juisi ya majani ya mpapai ina uwezo wa kutibu malaria na saratani, japokuwa tafiti hizo hazikukubawaliwa kisayansi.
Faida za kiafya za tunda la papai

KILIMO CHA MATANGO

ni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C
Udongo Hustawi vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba usiotuamisha maji
Maandalizi ya shamba Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45

Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi 1.5 kutoka kati ya tuta na tuta
Upandaji Zipo aina mbili za upandaji,
1.ya kwanza ni ile ya kupanda mbegu moja kwa moja na
2. ya pili ni ile ya kupanda mbegu katika trei na kuhamisha baada ya siku 8 hadi 10.
Njia ya kupanda mbegu moja kwa moja ni rahisi lakini ile ya kupanda katika trei ni bora zaidi kwani shamba hujaa vizuri katika nafasi na hukua haraka na kuzaa mavuno mengi
Pima mashimo ya kupandia katika umbali wa sentimita 20 hadi 25 kutoka shina hadi shina mstari mmoja kwa tuta na sentimita 40 katika mfumo wa zig-zag pande zote mbili za tuta na kupanda
Mbolea kianzio iwekwe katika kila shimo na kupanda endapo miche kutoka katika trei itatumika Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda

Palizi Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu.

MUONGOZO WA JINSI YA KULIMA PAPAI

UTANGULIZI
Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.
Uzalishaji wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili.
KUHUSU MPAPAI
Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu
i) Mpapai wenye maua kiume tu ii) Mpapai wenye maua kike tu iii) Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya)


Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.

SOMA HII INAWEZA KUKUSAIDIA KATIKA KUFIKIA MALENGO: KILIMO CHA PAPAI

HEBU CHUKUA KALUKUKETA YAKO, TUFANYE HESABU..!!

Eka moja ya shamba la papai inaweza kuingiza miche 1000-1200(elfu moja hadi elfu na mia mbili)-zile mbegu fupi. Tufanye umepanda miche 1,000. Mti mmoja ukiuhudumia vema unaweza kutoa matunda hadi 120 kwa msimu. Tufanye umetoa matunda 80, tu. Tunda moja kwa bei ya shamba tufanye umeuza bei ya "kutupwa" ya Tsh. 500/= (lakini papai lililoshiba linauzwa hadi Tsh. 3,000/= sokoni). Chukua 500/= mara 80 unapata 40,000/=(elfu arobaini kwa mti mmoja). Sasa chukua 40,000/= zidisha mara 1,000 unapata 40,000,000/=(milioni arobaini). Gharama za kulima papai ekari moja haizidi milioni mbili. Toka kupandwa hadi kuvunwa papai inachukua miezi kumi tu. Tufanye hivi: ukishavuna hii milioni 40 jibane, usiitumie, mwaka unaofuata nenda kapande tena papai ekari 20! Kama kalukuketa yako haisumbui utapata total ya Tsh. Milioni mia nane (800,000,000/=). Hapo nakuruhusu chukua milioni 100 zitumbue kwa raha zako(na mtu yeyote akikuhoji kwa nini unatumbua pesa nyingi namna hiyo?


 Mwambie Sanga kaniruhusu!), Then, milioni 200 wekeza tena shambani, halafu milioni 500 weka benki. Naishia hapa kuhusu "kukalukuketi", malizia mwenyewe uone kama utakosa milioni 890 ndani ya miaka mitano. Tuache hayo.