SOMA HII INAWEZA KUKUSAIDIA KATIKA KUFIKIA MALENGO: KILIMO CHA PAPAI

HEBU CHUKUA KALUKUKETA YAKO, TUFANYE HESABU..!!

Eka moja ya shamba la papai inaweza kuingiza miche 1000-1200(elfu moja hadi elfu na mia mbili)-zile mbegu fupi. Tufanye umepanda miche 1,000. Mti mmoja ukiuhudumia vema unaweza kutoa matunda hadi 120 kwa msimu. Tufanye umetoa matunda 80, tu. Tunda moja kwa bei ya shamba tufanye umeuza bei ya "kutupwa" ya Tsh. 500/= (lakini papai lililoshiba linauzwa hadi Tsh. 3,000/= sokoni). Chukua 500/= mara 80 unapata 40,000/=(elfu arobaini kwa mti mmoja). Sasa chukua 40,000/= zidisha mara 1,000 unapata 40,000,000/=(milioni arobaini). Gharama za kulima papai ekari moja haizidi milioni mbili. Toka kupandwa hadi kuvunwa papai inachukua miezi kumi tu. Tufanye hivi: ukishavuna hii milioni 40 jibane, usiitumie, mwaka unaofuata nenda kapande tena papai ekari 20! Kama kalukuketa yako haisumbui utapata total ya Tsh. Milioni mia nane (800,000,000/=). Hapo nakuruhusu chukua milioni 100 zitumbue kwa raha zako(na mtu yeyote akikuhoji kwa nini unatumbua pesa nyingi namna hiyo?


 Mwambie Sanga kaniruhusu!), Then, milioni 200 wekeza tena shambani, halafu milioni 500 weka benki. Naishia hapa kuhusu "kukalukuketi", malizia mwenyewe uone kama utakosa milioni 890 ndani ya miaka mitano. Tuache hayo.
Najua utaniuliza, maswali kuhusu soko, hali ya hewa, udongo, mbegu na mengine. Tafadhali hayo maswali tafuta majibu mwenyewe, (nimekuachia home work-usilete uvivu wa kutafuniwa kila kitu). Lakini ukilima mapapai ukakosa soko hapa nchini kuna nchi nahitaji sana kama vile Comoro na Madagascar. Kama umeungana na waliokariri kwamba hela ni ngumu zama hizi za mtumbua majipu, shauri yako, maana huo sasa ni uzembe laivu!
Kwa haya na mengine mengi usisahau Ku like page hii.

5 comments:

James Albert said...

Ahsante sana kiongozi kwa makala nzuri ,binafsi nitafanya home work yangu as an aspiring investor

Unknown said...

Nimeipenda sana blog yako na malengo yako, naomba rekebisha nsmba ya Ezekiel imekosewa. Imezidi Namba moja.

Unknown said...

Mbolea itakayo tumika kinyesi cha wanyama au ndege

Unknown said...

nashukuru kwa taarifa sahihinwaswahili walisema information is power nawe hukuwa mchoyo asanta sana

Unknown said...

Nashukuru kwa elimu